LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri OR-TAMISEMI aanzia kazi Mwanza “aacha maagizo mazito”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo John Dugange (mwenye tai anayepokea tofali) akishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika Zahanati ya Fumagila Kata ya Kishiriki jijini Mwanza baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa jengo la wazazi katika Zahanati hiyo uliogharibu shilingi milioni 137 zilizotolewa na Serikali.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo John Dugange (kushoto) pamoja na mbunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (kulia) wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika zahanati ya Fumagila jijini Mwanza.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo John Dugange (kushoto) pamoja na mbunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (kulia) wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika zahanati ya Fumagila jijini Mwanza.
Serikali ilitoa shilingi milioni 200 katika Zahanati ya Fumagila jijini Mwanza ambapo shilingi milioni 137 zilitumika kujenga jengo la wazazi na chechi iliyobaki imeanza kutumika kwenye ujenzi wa jengo la maabara katika zahanati hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo John Dugange aliwapongeza viongozi jijini Mwanza kwa kusimamia vyema ujenzi wa jengo la wazazi na chechi kubaki kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara na kuahidi kuwa Serikali itaongeza shilingi milioni 300 ili kujenga majengo mengine ili kuipandisha hadi zahanati hiyo kuwa Kituo cha Afya.
Ni kama wanasema "Hapa Kazi Tu"...
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo John Dugange (kushoto) akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula (kulia).
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo John Dugange pamoja na viongozi mbalimbali wakitoka kukagua ujenzi wa mashine ya kuchomea taka (Incinerator).
Mwonekano wa jengo la wazazi katika Zahanati ya Fumagila jijini Mwanza pamoja na msingi wa ujenzi wa jengo la maabara katika zahanati hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.