LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwimbaji Natacha kutoka Burundi afunga mwaka kivingine

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Akiwa ni mwimbaji mashuhuri anayewakilisha nchini Burundi Natacha Ngendabanka ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa kitamaduni na kuhamasisha Cica International Festival 2014.

Natacha ambaye anaiwakilisha vyema nchi ya Burundi kupitia muziki na kujituma kwake ni jambo ambalo limemfanya kuthubutu zaidi kuwafikia wasanii kutoka nchi mbali mbali na kufanya nao kazi zake za muziki akiwa ana imba miondoko ya kiafrika zaidi na baadhi ya wasani ambao amefanya nao kazi ni pamoja na fally ipupa kutoka nchini congo,sheebah kutoka nchini Uganda, Fik FFameica kutoka nchini Uganda na kutoka Tanzania Natacha amefanya kazi na Barnaba classic. 

Vilevile Natacha amekuwa na ari kubwa ya kuipeperusha bendera ya taifa la Burundi kupitia sanaa yake kiasi ambacho kilipelekea kuwa msanii pendwa kwa rais wa nchi hiyo hayati Pierre Nkurunziza. Mwaka 2020 Natacha ameachia kazi kadhaa ikiwemo zunza ambayo imefankiwa kwa kiasi kikubwa kufanya vyema na sasa ameamua kufunga mwaka na wimbo wake mpya ambao ameshirikiana na msanii kutoka nchini Kenya Femi One moja kati ya msanii ambaye mwaka huu amaefanya vizuri na wimbo wake maarufu utawezana. 

Lakini jambo zuri na la pekee kuhusu wimbo huu mpya wa Natacha shikisha ni wimbo ambao ametumia lugha ya kiswahili mwanzo mpaka mwisho pasipo kuchanganya na kirundi kama ambavyo imezoeleka kwa msanii huyo. 

Karibu kutazama wimbo huo na unaweza kumfatilia Natacha katika kurasa zake za kijamii kwa jina la @natachaburundi.
Imeandaliwa na Natty E Brandy

No comments:

Powered by Blogger.