LIVE STREAM ADS

Header Ads

MISUNGWI: Mwenyekiti wa Halmashauri akataa Hati chafu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Diwani wa Kata ya Usagara Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Erasto Kashinje ameidhinishwa kwa kura zote za ndiyo na baraza la madiwani kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo akirithi mikoba ya Antony Bahebe.

Baada ya kuidhinishwa, Kashinje akaahidi kuwa atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha Halmashauri inasimamia vyema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na ukusanyaji mapato na kwamba dhamira ni kuona Halmashauri hiyo ikipata hati safi kila mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kilichokezi Disemba 07, 2020.
Awali Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Misungwi, Rahma Fidel kutoka Kata ya Bulemeji akiomba kuidhinishwa na madiwani kushika nafasi hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.