Tamasha la utoaji zawadi jijini Mwanza, rekodi yawekwa CCM Kirumba
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeandaa Tamasha la Utoaji Zawadi kwa Waalimu na Shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba waliohitimu mwaka 2020 na matokeo kutangazwa mapema mwaka huu 2021 ambapo ilishika nafasi ya tatu kitaifa.
Mgeni rasmi kwenye tamasha hilo lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi Januari 23, 2021 alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI. Katika tamasha hilo viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa idara, madiwani na watendaji walishiriki pamoja michezo mbalimbali ingawa mchezo wa soka ulivuta hisia za wengi.
Mgeni rasmi akikagua timu, wakuu wa idara wakiongozwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza pamoja na madiwani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari za Matamasha mbalimbali
No comments: