LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jumuiya ya LVRLAC yahimiza utunzaji mazingira ya Ziwa Victoria

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mamlaka za Serikali za Mitaa katika nchi za Tanzania, Uganda na Kenya zimehimizwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria (LVRLAC) katika kutunza mazingira ya Ziwa Victoria ikiwemo kupambana na magugu maji.

Rai hiyo imetolewa jijini Mwanza kwenye mkutano wa jumuiya ya LVRLAC Kanda ya Tanzania ambao kando ya kuangazia mikakati ya kutunza mazingira ya Ziwa Victoria, pia umejadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya jumuiya wanachama katika kuchochea maendeleo ya pamoja.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa LVRLAC Kanda ya Kenya, Richard Ogindo akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa LVRLAC Afrika Mashariki ambapo amehimiza wanachama wa umoja huo kuchangia utekelezaji wa shughuli mbalimbali bila kutegemea wafadhili pekee.
Mwenyekiti wa LVRLAC Kanda ya Tanzania, William Gumbo amesema jumuiya hiyo imesaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi bilioni 20 ikihusisha mazingira, maji na afya.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria (LVRLAC) ilianzishwa mwaka 1997 ili kuchagiza kwa  pamoja mikakati ya utunzaji mazingira ya Ziwa Victoria pamoja na fursa mbalimbali za maendeleo katika jumuiya.
Katibu Mkuu Jumuiya ya Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria (LVRLAC) Kanda ya Tanzania akieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na jumuiya hiyo ambazo ni pamoja na kuweka mikakati ya utunzaji mazingira ya Ziwa Victoria.
Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria (LVRLAC) Kanda ya Tanzania umefanyika kwa siku tatu jijini Mwanza ukitanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwemo ziara ya kimafunzo katika miradi ya kimkakati katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Wadau mbalimbali wameshiriki mkutano huo ikiwemo Benki ya NMB ambayo imeahidi kushirikiana na Jumuiya ya Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria (LVRLAC) katika utekelezaji wa shughuli zake.
Wajumbe mbalimbali wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria (LVRLAC) Kanda ya Tanzania wakifuatilia mkutano huo ambao pia umeambatana na uchaguzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.