LIVE STREAM ADS

Header Ads

UPDATES kutoka Dodoma ilikotokea ajali ya Treni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Treni hiyo mali ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ilikuwa na abiria 720 ambapo abiria watatu wamefariki dunia huku abiria 66 wakijeruhiwa, hii ikiwa ni kwa mjibu wa Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amewatembelea majeruhi wa ajali ya treni katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma ambapo ameagiza viongozi mkoani humo kuhakikisha wanasimamia zoezi la kuwafikisha makwao majeruhi wote baada ya kupata ahueni.

Mama Samia ameyasema hayo Januari 03, 2021 baada ya kuwatembelea majeruhi wa ajali hiyo iliyotolea Januari 02, 2020 majira ya saa moja kasorobo jioni katika eneo la Bahi mkoani Dodoma ikitokea jijini Dar es salaam kuelekea mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Mwanza ambapo ameeleza kuridhishwa na hali zao pamoja na huduma wanazopatiwa hospitalini hapo.

Pia amewajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa Dodoma, General.
Tazama BMG TV hapa chini
Imeandaliwa BMG kwa msaada wa mitandao mbalimbali

No comments:

Powered by Blogger.