LIVE STREAM ADS

Header Ads

Meya Sima atoa masaa 24 kwa mfanyabiashara jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima (kushoto) ametoa muda wa masaa 24 kwa mfanyabiashara Sajady Ahmad (kulia) awe amevunja jengo alilolijenga katika Mtaa wa Nera bila kufuata taratibu. 

Meya Sima ametoa agizo hilo mapema Januari 08, 2020 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali jijini Mwanza, baada ya kufika katika eneo la jengo hilo lililopo katika kiwanja namba 15 block B mali ya Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Alisema baada ya mfanyabiara huyo kupata idhini ya kuwekeza katika eneo hilo, alianza ujenzi bila kuwa na vibali pamoja na kukiuka sheria ya mipango miji inayotaka maeneo ya katikati ya Jiji kujengwa majengo ya ghorofa na si majengo mafupi kama alivyofanya. 

Aidha aliongeza kuwa Disemba 03, 2020 mfanyabiashara huyo alipokea barua ya kusitisha ujenzi huo lakini alikaidi na kuendelea hadi hatua ya upauaji aliyofikia sasa na kwamba akishindwa kubomoa hilo Halmashauri ya Jiji la Mwanza italibomoa na kisha atalipa gharama za ubomoaji. 

Katika hatua nyingine Meya Sima aliwaonya wale wote wanaoendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali bila kuwa na vibali kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kueleza kuwa zoezi la ukaguzi wa majengo yasiyo na vibali ni endelevu na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukiuka taratibu za ujenzi. 

Kwa upande wake mfanyabiashara huyo alijitetea kwamba aliendelea na ujenzi licha ya kutakiwa kusitisha ujenzi huo baada ya kupata ridhaa kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ingawa alipotakiwa kuonyesha kibali cha maandishi alichopewa na mtumishi huyo hakukionyesha na wala hakuwa tayari kumtaja majina yake.
Na Michael Jamson, Mwanza
Sehemu ya mwonekano wa jengo hilo lililopo Mtaa wa Nera Kata ya Isamilo jijini Mwanza.
Mwonekano wa jengo hilo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima akiwa na viongozi mbalimbali jijini Mwanza alipofika kukagua jengo hilo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima akiwa na viongozi mbalimbali jijini Mwanza wakikagua jengo hilo ambalo limejengwa kwa mfumo wa stoo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima akiwa na viongozi mbalimbali jijini Mwanza wakiwa kwenye jengo hilo lililojengwa kwa ramani fupi badala ya ghorofa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima akiwa na viongozi mbalimbali jijini Mwanza wakikagua jengo hilo lililojengwa kwa mfumo wa stoo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima akitoka kukagua jengo hilo ambalo inaelezwa ujenzi wake umekiuka taratibu ikiwemo kutumia ramani ya nyumba fupi badala ya ghorofa katika sheria ya mipango miji inavyoelekeza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Costantine Sima (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali jijini Mwanza alipotembelea ujenzi wa jengo hilo Mtaa wa Nera.

No comments:

Powered by Blogger.