LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tunalenga wahitimu wetu wajiajiri, wasitegemee kuajiriwa- SAUT

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT kimeweka bayana kwamba wajibu wake ni kuzalisha wahitimu wenye ujuzi wa kuwasaidia kujiajiri na si kutegemea kuajiriwa pekee na hivyo kujibu changamoto ya ukosefu wa ajira ambayo imekuwa ikilalamikiwa katika jamii.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na mahafali ya 22 ya chuo hicho kampasi ya Malimbe jijini Mwanza yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa Januari 29, 20221.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu akitoa taarifa kuhusiana na mahafali ya 22 yanayotarajiwa kufanyika Januari 29, 2021.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu na menejimenti ya chuo hicho wakielekea kwenye maonesho ya kitaaluma (SAUT Community).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Balozi Profesa Costa Ricky Mahalu akifungua maonyesho ya kitaaluma (SAUT Community).
Maonesho ya kitaaluma (SAUT Community yakiendelea katika viunga vya Raila Odinga.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.