LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kuelekea miaka 44 ya CCM, UVCCM Nyamagana washiriki ujenzi wa Shule mpya ya Bulale

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza umesema utahakikisha unashirikiana na viongozi wa Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa vyumba vya madarasa na si kusubiri hadi Rais Dkt. John Pombe Magufuli atoe maagizo kama ambavyo imekuwa ikitokea katika mikoa mingine.

Viongozi wa umoja huo wameyasema hayo Januari 26, 2020 waliposhiriki kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bulale iliyopo Kata ya Buhongwa jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 44 ya CCM, Februari 05, 2021.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Vijana wa UVCCM wilayani Nyamagana wakishiriki nguvu kazi kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bulale jijini Mwanza.
Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Malanyingi Matukuta akishirikiana na vijana wa umoja huo kwenye ujenzi wa shule hiyo.
Kukamilika kwa Shule ya Sekondari Bulale kutasaidia kuondoa msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari Buhongwa.
UVCCM wilayani Nyamagana wakichapa kazi kwenye ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Bulale iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
UVCCM wilayani Nyamagana wakishusha mbao kwa ajili ya upauaji wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Bulale.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.