LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waliokimbia ukeketaji wasimulia, walivyotoroka, ombi kwa Magufuli

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wasichana waliokimbia ukeketaji mkoani Mara katika msimu wa mwaka 2020/21 wameanza kurejea majumbani ili kuendelea na masomo japo miongoni mwao wamejawa na hofu kutokana na baadhi ya wazazi kutokuwa tayari kuwapokea.

Wasichana hao ni wale waliokimbilia katika vituo vya nyumba salama vilivyopo wilaya za Butiama (wasichana 166) na Serengeti (wasichana 53) mkoani humo chini ya shirika la Hope for Girls & Women in Tanzania.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa shirika la Hope for Girls & Women in Tanzania, Rhobi Samwel akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwaaga wasichana/ mabinti waliokimbia ukeketaji mkoani Mara.
Mkurugenzi wa shirika la Hope for Girls & Women in Tanzania, Rhobi Samwel akieleza shughuli zinazofanywa na shirika hilo katika kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji.
Wadau/ viongozi mbalimbali.
Baadhi ya wasichana. mabinti waliokimbia ukeketaji mkoani Mara.
Mdau wa maendeleo, Mataro Mwita (kulia) akiwa kwenye picha na baadhi ya wasichana waliokimbia ukeketaji mkoani Mara alipohudhuria hafla ya kufunga kambi baada ya msimu wa ukeketaji 2020/21 kufikia tamati.
Kutokana na jitihada za wadau mbalimbali ikiwemo utoaji elimu hadi ngazi ya jamii, kasi ya ukeketaji imeendelea kupungua katika maeneo mengi nchini ikiwemo mkoani Mara.
Baadhi ya wasichana waliokimbia ukeketaji mkoani Mara wakiwa kwenye hafla ya kufunga kambi ili kurejea majumbani kuendelea na masomo baada ya msimu wa ukeketaji 2020/21 kufikia tamati.
Mkurugenzi wa shirika la Hope for Girls & Women in Tanzania Rhobi Samwel (kushoto), Mdau wa maendeleo, Mataro Mwita (kulia) na baadhi ya watoto waliokimbia ukeketaji.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.