LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB yatoa zawadi kwa wanafunzi bora Chuo Kikuu cha SAUT

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya CRDB imekabidhi zawadi za ngao kwa wahitimu wawili kutoka Chuo Kikuu cha SAUT waliopata ufaulu wa juu katika kitivo cha uhasibu na fedha na kitivo cha utawala wa biashara waliohitimu mwaka wa masomo 2020/21.

Wahitimu hao ni Godlina Kimaro kutoka kitivo cha uhasibu na fedha pamoja na Rehema Maige kutoka kitivo cha utawala wa biashara ambaye pia ni mwanafunzi bora wa jumla aliyepata ufaulu wa juu kwa vitivo vyote.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwenye mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu SAUT kampasi kuu ya Mwanza, Meneja wa CRDB tawi la SAUT, Hezron Ikelesho alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono mchango wa wanafunzi wa chuo hicho ambao fedha zao ikiwemo kutoka bodi ya mikopo zinapitia CRDB.

Wanafunzi wengine waliofanya vizuri na vitivo wanavyotoka kwenye mabano ni Nimrodi Jotham (Education), Sabina Misala (Social Science and Communication), Rose Morice (Law).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mmoja wa wahitimu wa Chuo Kikuu SAUT, Rehema Maige aliyefanya vizuri kwenye 'Faculty of Business Administration' na pia 'The Best overall student'.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.