LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wahitimu SAUT watakiwa kuwa waadilifu “msiende ku-bet”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT wametakiwa kuitumia vyema elimu waliyoipata katika kujiajiri na kuajiriwa badala ya kwenda kufanya matendo yasiyo mema ikiwemo wizi na michezo ya kamari (betting) kwani wasipofanya hivyo watakuwa wasomi wapumbavu.

Mkuu wa Wilaya Sengerema, Emmanuel Kipole aliyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo ya 22 yaliyofanyika Januari 29, 2021 katika viunga vya Chuo cha SAUT Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu SAUT, Askofu Flavian Kasala akizungumza kwenye mahafali hayo.
Jumla ya wahitimu 2,500 walihitimu masomo yao katika ngazi mbalimbali chuoni hapo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.