LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB kuwezesha ujenzi wa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Uongozi wa Benki ya CRDB umeeleza kuwa utaendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya tano kutoka Mwanza hadi Isaka Shinyanga unafanikiwa kama ilivyopangwa hatua ambayo itasaidia pia kukuza fursa za kiuchumi nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela aliyasema hayo jijini Mwanza wakati wa kongamano la kujadili mpango kazi na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF).

Nsekela alisema benki hiyo itahakikisha inaendelea kuweka mikakati thabiti itakayosaidia Serikali, wakandarasi na wazabuni mbalimbali kutekeleza ipasavyo miradi mbalimbali ya kimkakati nchini ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli hiyo ya kisasa.

"Uwezeshaji tunaoufanya ni wa moja kwa moja katika miradi mbalimbali ambapo mwaka juzi tulifanya uwezeshaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 40 na pia tutakuwa tunawawezesha wakandarasi na wazabuni kwa maana ya kuwapa mikopo ya utekelezaji wa miradi hiyo" alisema Nsekela na kuongeza;

"Tunatoa mikopo ya utekelezaji wa kandarasi/ zabuni bila dhamana yoyote kupitia huduma zetu za ‘Purchase Order Financing’ na ‘Invoice Discounting’ ili kusaidia wakandarasi na wazabuni wazawa kutekeleza miradi hiyo kwa weledi, ufanisi na kupata matokeo chanya yenye kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa taifa letu" alisisitiza Nsekela.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini na kuwataka wakandarasi kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo katika kukuza na kuboresha utendaji wa kazi zao.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, pamoja na mengine aliwahakikishia ulinzi na usalama wa vifaa kwa muda wote ambao wakandarasi na wazabuni mbalimbali watakuwa wakitekeleza mradi huo na hivyo kuondoa mwanya wa wizi wa vifaa vya ujenzi.

Pia Mongella aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimakati nchini ukiwemo mradi wa SGR huku akiongeza kuwa fursa zinazotolewa na benki hiyo zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Masanja Kadogosa alisema mradi huo mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa (SRG) kutoka Mwanza hadi

Isaka utaigharimu Serikali kiasi cha shilingi trioni tatu, kutoa fursa za ajira rasmi kwa wafanyakazi wapatao 15,000 na ajira za muda 75,000 ambapo unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miezi 18 na kampuni ya China Civil Engineering Constructions Commpany (CCECC).

Aidha Kadogosa alisema mbali na fursa hizo za ajira pia mradi huo wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka yenye urefu wa kilomita 249 utatoa fursa za uzalishaji wa zabuni mbalimbali ikiwemo usafirishaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na vyakula kwa wananchi hivyo wachangamkie fursa hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na wanahabari kuhusiana na mchango wa benki hiyo kwenye kuwezesha utekelezaji wa mradi wa SGR kuanzia Mwanza hadi Isaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Abdulmajid Nsekela akizungumza kwenye mkutano wa kujadili mpango kazi na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye ujenzi wa reli ya kisasa SGR kuanzia Mwanza hadi Isaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Francis Nanai alisema ni muhimu wa sekta binafsi kushiriki kwenye utekelezaji wa mradi wa SGR hivyo wananchi wachangamkie fursa zilizopo ikiwemo  usafirishaji wa vifaa vya ujenzi.
Wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa walishiriki kongamano hilo lililofanyika jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula akizungumza kwenye mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
Kongamano la kujadili la kujadili mpango kazi na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka lilidhaminiwa na benki ya CRDB.
Meneja Biashara benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly akifuatilia kongamano hilo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na Meneja Biashara benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitembelea mabanda ya wanawake wajasiriamali ambao wamekuza biashara zao kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa na benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki hiyo itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo kwa ajili ya kuboresha shughuli zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alipotembelea mabanda ya wanawake wajasiriamali walionufaika na huduma za CRDB katika kukuza biashara zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanawake wajasiriamali jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiteta jambo na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, na wanawake wajasiriamali jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.