LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenyekiti Tume ya Madini avutiwa na kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse (kushoto) baada ya kutembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu (Gold Refinery) kinachojengwa jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula (kulia) akizungumza jambo baada ya kutembelea ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza na kuridhishwa na maendeleo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Samamba pamoja na watendaji na makamishna wengine wa tume hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya pamoja ya ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu, Deusdedith Magala (kulia) akitoa maelezo kuhusiana na ujenzi huo ambao hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 10.
Kamishna wa Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki (kushoto) akihimiza watanzania kujifunza ujuzi na utaalamu wa kuendesha mitambo mbalimbali iliyosimikwa kwenye kiwanda hicho ili kuwa na uwezo wa kuisimamia vyema.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali alioambatana kwenye ziara hiyo ya kutembelea ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula ametembelea ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu (Gold Refinery) kinachojengwa jijini Mwanza na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.

Prof. Kikula akiwa ameambatana na watendaji na makamishna mbalimbali wa Tume ya Madini ametembelea kiwanda hicho Februari 12, 2021 na kueleza kuwa kukamilika kwake kutatengeneza sifa na historia kubwa kwa Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa, Dkt. Venance Mwasse amesema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kusafisha kilo 480 za dhahabu kwa siku hadi kufikia ubora wa asilimia 99.99 na kuongeza mapato kwa Serikali.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.