LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella ameba sakata la Mjane aliyeuziwa nyumba “atoa siku tatu”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Hatimaye kilio cha miaka mingi cha mjane Prucheria Balilemwa (79) mkazi wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza kulalamikia nyumba yake kuuzwa kinyume cha utaratibu kimesikika ambapo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella Jumapili Februari 14, 2021 ameagiza mama huyo arejeshewe hati ya nyumba hiyo. 

Mongella amefika nyumbani kwa mjane huyo na kuagiza hadi kufikia Jumatano Februari 17, 2021 awe amepata hati ya nyumba hiyo ili amkabidhi mjane huyo kwani mazingira ya nyumba hiyo kuuzwa yanatia mashaka. 

Mjane huyo ameomba Serikali imsaidie ili mfanyabiashara Riziki Mbise maarufu kwa jina la Mambo ya Chinga anayedaiwa kununua nyumba hiyo na kisha kuibomoa upande mmoja wa mbele amjengee nyumba yake. 

Inaelezwa kuwa nyumba hiyo iliuzwa mwaka 2003 kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya mmewe Poncian Balilemwa aliyefariki dunia mwaka 1995 kushindwa kulipa deni alilokopa benki mwaka 1984. Malalamiko hayo ya muda mrefu pia yalimfikia Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyeagiza yashughulikiwe haraka.
#BMGBlog
Mama huyo ameomba Serikali imsaidie ili mfanyabiashara Riziki Mbise maarufu kwa jina la Mambo ya Chinga aliyenunua nyumba hiyo na kisha kuibomoa upande mmoja wa mbele aijenge.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.