LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtangazaji hakuwa na la kusema, Simba ikipata goli. Refa na penati ya wazi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Timu ya Soka ya Simba kutoka Tanzania, imeendelea kutamba kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuwatandika washindi wa tatu wa Klabu za Soka Duniani Al Ahly kutoka Misri kwa bao 1-0 kwenye dimba la Mkapa jijini Dar, Februari 23, 2021.

Huu ni mchezo wa pili kwa Simba kushinda baada ya ule wa ugenini ilipoitungua tena AS Vita ya Congo kwa bao 1-0 ugenini.

Kwa ushindi huo, Simba wanarejea kileleni katika kundi A baada ya kufikisha pointi sita wakifuatiwa na AS Vita wenye pointi tatu sawa na Al Ahly ambayo ipo nafasi ya tatu na ina pointi tatu huku Al-Merriekh ikiwa nafasi ya nne ikiwa haina pointi hata moja.

No comments:

Powered by Blogger.