LIVE STREAM ADS

Header Ads

Madiwani Mwanza wataka miradi ikamilike kwa wakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango inayoundwa na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo ikiwemo ya afya, elimu na ile ya kimkakati na kushauri ikamilike kwa wakati ili kutoa huduma kwa wananchi.

Ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo ilifanyika Februari 23, 2021 ikianzia Zahanati ya Isamilo na wajumbe kuhimiza Mkurugenzi wa Halmashauri aidhinishe fedha zinazohitajika ili kukamilisha mfumo wa maji, kichomea taka pamoja na uzio ili ianze kufanya kazi kwani jengo limekamilika muda mrefu na lisipoanza kutumika linaweza kuchakaa mapema.

Pia kamati hiyo ilikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Nyakabungo, madarasa ya vyumba sita katika shule ya msingi Mabatini, bweni la wasichana katika shule ya sekondari Nyanza, uanzishwaji wa shule ya msingi ya kiingereza Nyanza, vyumba vya madarasa na bweni la wasichana katika shule ya sekondari Buhongwa, soko la kisasa Mwanza pamoja na Stendi ya kisasa Nyegezi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ujenzi wa Zahanati ya Isamilo.
Diwani wa Kata ya Isamilo, Charles Nyamasiriri (wa pili kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Isamilo na kueleza kuwa wananchi wanapata adha ya kufuata huduma za afya mbali hivyo ni vyema Zahanati hiyo ikaanza kutoa huduma.
Kamati pia ilikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Nyakabungo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Julius Mlongo (kushoto) akiongoza msafara wa wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango kukagua miradi ya maendeleo.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati ikipata taarifa ya uendeshaji Nyanza English Medium iliyotokana na shule kongwe ya msingi Nyanza.
Maendeleo ya jenzi wa soko la kisasa Mwanza.
Ujenzi wa soko kuu Mwanza umefikia asilimia 18 na changamoto kubwa ni uwepo wa maji hivyo mkandarasi ametakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi ndani ya miezi 18 kuanzia mwaka 2020.
Ujenzi wa soko la kisasa Mwanza ukiwa hatua ya awali ya msingi.
Maendeleo ya ujenzi wa soko la kisasa Mwanza ambapo hadi kukamilika litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 20, fedha zote zikitolewa na Serikali Kuu.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwasili shule ya sekondari Mwanza kukagua bweni la wasichana ambalo limekamilika tayari.
Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitoa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Nyanza.
Bweni la wasichana katika shule ya wasichana Mwanza limekamilika na wanafunzi tayari wanalitumia na kuondoa adha ya msongamano iliyokuwepo awali.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mabatini.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango waliagiza maboma haya yakamilike ili wanafunzi wayatumie yakiwa kwenye hali nzuri.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.