Uzinduzi wa ‘Mzigo Ulioboreshwa’ jijini Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Uzinduzi huo umefanyika Alhamisi Februari 25, 2021 katika tawi la CRDB tawi la Rock City jijini Mwanza ikiwa ni masaa machache baada ya uzinduzi wa kitaifa ufanyika usiku wa Februari 24, 2021 jijini Dar es salaam.
Kufuatia huduma hiyo, sasa wateja wa benki ya CRDB wataweza kujifungulia wenyewe akaunti zao wakiwa popote, kununua/ kilipia bima za mali zao, kupata taarifa za miamala ya akaunti zao pamoja na kuimarisha usalama wa fedha zao pia.
Aidha wataweza kufanya miamala na kulipia bidhaa mbalimbali popote walipo, kupata mikopo rahisi na huduma mbalimbali kupitia mawakala ama mashine za ATM bila kuwa na kadi za benki.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama picha za awali za watumishi na wateja wa CRDB kwenye uzinduzi huo unaofanyika katika tawi la benki hiyo lililopo Rock City Mall jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> Habari zaidi kuhusiana na CRDB
No comments: