LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIDEO: Maendeleo ya ujenzi wa Stendi ya kisasa Nyegezi Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ujenzi wa jengo la abiria na kitega uchumi katika stendi ya kisasa Nyegezi jijini Mwanza umefikia asilimia 18 ambapo hadi kukamilika utagharibu fedha za Serikali kiasi cha shilingi bilioni 15.8.

Mradi wa stendi ya Nyegezi unaotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia kampuni ya Mohammed Bulders ulianza Septemba 2020 ukitarajiwa kukamilika Aprili 2022 ikiwa na uwezo wa kuchukua mabasi 120 kwa wakati mmoja, maduka 85, kumbi za burudani, maeneo matatu ya abiria kukaa.

Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza chini ya Mwenyekiti wake Zebedayo Athuman imetembelea mradi huo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 tangu kuasisiwa chama hicho. Pia Kamati hiyo imetembelea tenki la mradi wa maji Butimba-Sahwa na kuagiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili kutoa huduma kwa wananchi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.