LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya Siasa CCM Nyamagana yakagua ujenzi wa Stendi Nyegezi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza imekagua maendeleo ya ujenzi wa stendi ya kisasa Nyegezi na tenki la mradi wa maji Sahwa-Butimba jijini Mwanza na kuagiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati ili kutoa huduma kwa wananchi.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Nyamagana, Zebedayo Athumani amesema ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 tangu CCM iasisiwe Februari 05, 1977.

Naye Katibu wa CCM Wilaya Nyamagana, Geofrey Kavenga amesema chama hicho kina wajibu wa kuisimamia Serikali ili kuhakikisha inasimamia vyema miradi ya maendeleo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Nyamagana, Zebedayo Athumani akizungumza jambo baada ya kutembelea mradi wa Stendi ya Nyegezi.
Katibu wa CCM Wilaya Nyamagana, Geofrey Kavenga akitoa salamu zake wakati wa ziara hiyo.
Katibu Tawala Wilaya Nyamagana, Yonas Alfred akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi.
Sehemu ya mwonekano wa jengo la kusibiria abiria pamoja na shughuli mbalimbali za kibiashara linalojengwa katika stendi ya kisasa Nyegezi ambayo hadi kukamilika itagharimu shilingi bilioni 15.8.
Ujenzi wa jengo la abiria ukiendelea kwenye mradi huo wa stendi ya kisasa Nyegezi.
Tenki la mradi wa maji Butimba-Sahwa jijinu Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.