LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tume ya Madini yashiriki Maonesho ya Mkutano wa Kimataifa wa Madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Leo tarehe 21 Februari, 2021 Tume ya Madini imeanza ushiriki wake katika maonesho yanayoendelea jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Madini unahusisha wadau wa madini ikiwa ni pamoja na Taasisi za Serikali, Taasisi za Kifedha, kampuni za uchimbaji wa madini, wachimbaji wadogo wa madini, wafanyabiashara wa madini.
Na Greyson Mwase, Dar
Kaimu Mtendaji Mkuu Tume ya Madini, Mhandisi Yahaya Samamba (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji mbalimbali wa Tume hiyo.
Kaimu Mtendaji Mkuu Tume ya Madini, Mhandisi Yahaya Samamba (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji mbalimbali wa Tume hiyo.
Mkutano wa Kimataifa wa Madini umeanza Februari 21-23, 2021 jijini Dar es salaama ambapo unatarajiwa kufunguliwa rasmi Februari 22, 2021 na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (hayuko pichani).

No comments:

Powered by Blogger.