LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajumbe RCC Mwanza wavutana mchakato wa kuanzisha wilaya mpya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa Mwanza wamevutana kuhusiana na mgawanyo wa maeneo ya utawala yanayopendekezwa kuunda wilaya mpya ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020.

Katika kikao hicho kilichoketi Februari 26, 2021 mvutano mkubwa ulikuwa kwenye baadhi ya Kata ikiwemo Kata ya Usagara iliyopo Wilaya Misungwi ambayo wajumbe kutoka Nyamagana walitaka isiende wilaya mpya bali iingie Nyamagana huku wakipingwa vikali na wajumbe kutoka Misungwi.

Pia Kata ya Nyamhongolo wilayani Ilemela ilileta mvutano baada ya wajumbe kutoka wilaya hiyo kutaka isiende wilaya mpya ambayo imependekezwa iitwe Bujora ama Kisesa.

Mwenyekiti wa Kikao hicho, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella licha ya kupokea mapendekezo ya wajumbe hao, alishauri mapendekezo yaliyotolewa na Sektretarieti ya Mkoa (RS) yafikishwe katika ngazi ya maamuzi kama yalivyo kwa ajili ya uamuzi zaidi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (kushoto) akiozoza kikao hicho. Katikati ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza Emmanuel Tutuba na kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza.
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Erasto Kashinje akizungumza kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine akifuatilia kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akiweka kumbukumbu kwenye kikao hicho.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.