LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mfanyabishara Tarime aendelea kusota rumande

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mfanyabiashara Lucas Sotel Ghati mkazi wa Tarime mkoani Mara anayekabiliwa na tuhuma za mauaji amepandishwa kizimbani Machi 05, 2021 ikiwa ni kwa mara nne.

Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kumsababishia kifo kijana aliyefahamika kwa jina la Wankuru Nyamuhanga Agosti 09, 2014 katika Kijiji cha Buriba wilayani Tarime.

Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Staff Sajent Bukuru Bukombe alimwambia Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Veronika Mugendi kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi itakapotajwa tena Machi 19, 2021 na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu.
Na Helena Magabe, Tarime

No comments:

Powered by Blogger.