LIVE STREAM ADS

Header Ads

Meya Mwanza aguswa na miradi ya vijana, lengo letu wapate mikopo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
    Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sima Costantine amefurahishwa na jitihada za uzalishaji mali zinazofanywa na vijana mbalimbali baada ya kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kupitia ufadhili wa shirika la Plan International.

Amesema Halmashauri ya Jiji la Mwanza itaendelea kutoa mikopo isiyo na riba kupitia mapato yake ya ndani ili kuhakikisha vijana hao wanaanzisha na kuendeleza miradi yenye tija baada ya kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo usindikaji bidhaa, kilimo na ufundi.

Sima aliyasema hayo Machi 16, 2021 baada ya kuwatembelea vijana wanaopata mafunzo ya usindikaji bidhaa na wale wanaojihusisha na kilimo kupitia mradi wa Vijana, Maisha na Kazi unaotekelezwa na shirika la Plan International kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo SIDO, VETA na TAHA.

Meneja mradi wa vijana, maisha na kazi kutoka Plan International, Nelson Msikula alisema mradi huo wa miaka minne tangu mwaka 2019 unalenga kuwafikia vijana zaidi ya elfu moja kwa lengo la kuwapatia ujuzi na mafunzo mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.

Katika ziara hiyo, Meya Sima pia aliambatana na mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula pamoja na wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza inayoongozwa na Mwenyekiti wake Skitu Senziote.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (wa nne kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali walipotembelea shamba daraja la kikundi cha vijana katika eneo la Malimbe walionufaika na mafunzo kupitia shirika la Plan International.
Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula (kulia) akifuatilia maelezo namna Plan International inavyowasaidia vijana kujikita kwenye shughuli za kilimo.
Shamba darasa la kikundi cha Young Adult kilichopo Malimbe jijini Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (wa tatu kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali walipotembelea vijana wanaopata mafunzo ya usindikaji bidhaa katika shirika la SIDO kupitia ufadhili wa shirika la Plan International.
Vijana wanaopata mafunzo SIDO Mwanza.
Vijana wanaopata mafunzo SIDO Mwanza wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Skitu Senziote.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Skitu Senziote ametoa pongezi kwa Plan International kwa jitihada zake za kuwajengea uwezo vijana kujitegemea kiuchumi.
Meneja Miradi kutoka shirika la Plan International Mkoa Mwanza, Majani Rwambali akieleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo katika kuchochea maendeleo.
Meneja Mradi wa Vijana, Maisha na Kazi kutoka shirika la Plan International, Nelson Msikula akieleza namna mradi huo umewanufaisha vijana (ke & me) tangu ulipoanza mwaka 2019 ambapo unatarajiwa kufikia tamati mwakani 2022.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.