LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia Suluhu Hassan aanzia TPA, ampa angalizo Waziri Jafo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Jumapili Machi 28, 2021 ameanza rasmi majukumu yake kwa kupokea ripoti za CAG na TAKUKURU kwa mwaka wa fedha 2019/20 na kueleza kuwa ripoti hizo zimebaini ubadhilifu katika mashirika kadhaa ya umma.

Baada ya kupokea ripoti hizo ameagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi huku akimtaka Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo kusimamia vyema fedha za miradi zinazotolewa na Serikali kwani wizara hiyo nayo imejaa ubadhilifu.

Rais Samia aliapishwa kushika wadhfa huo kwa mujibu wa Katiba baada ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufariki duniani Machi 17, 2021. Hapo awali alikuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.