LIVE STREAM ADS

Header Ads

Hafla kabambe ya kumuaga Mstaafu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kikundi cha Kusaidiana cha Wanawake Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa Mwanza (RS Boma Wanwake) kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2021 pamoja na kumuaga mwanachama mwenzao, Grace Kuhaba (kulia) ambaye amefikia umri wa kustaafu utumishi wa umma.

Hafla hiyo ilifanyika katika fukwe za Bonasera jijini Mwanza ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliyewahimiza wanawake hao kuendelea kweka juhudi katika kutimiza majukumu yao ya kuanzia ofisini hadi kwenye familia zao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo akiwahimiza zaidi wanawake kuhakikisha wanatimiza vyema majukumu yao hususani kusimamia maadili ya familia na kusomesha watoto ili nao wafikie ngazi mbalimbali za kiuongozi.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akitoa salamu kwenye hafla hiyo.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emmanuel Tutuba alihimiza watumishi kujiunga na kikundi hicho cha RS Boma Wanawake ili kusaidiana kwenye shughuli mbalimbali.
Wanachama wa kikundi cha RS Boma Wanawake wakitoa zawadi kwa mwenzao, Grace Kuhaba ambaye amestaafu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella aliungana na watumishi wake kufurahia muziki kwenye hafla hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.