LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake watoa changamoto kwa wanaume, wanajengeana nyumba za kisasa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wanawake kupitia vikundi vyao katika Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, wamewavutia wengi baada ya kuanzisha utamaduni mpya wa kuchangiana vifaa vya ujenzi pamoja na kushiriki nguvu kazi pindi mmoja wao anapoanza ujenzi.

Tayari nyumba zaidi ya 100 zimejengwa na vikundi mbalimbali vya wanawake wilayani humo hatua ambayo baadhi ya wadau wanasema ni vyema ikawahamasisha pia na wanaume ili kwa pamoja wasaidizaje na wake zao kuboresha makazi katika familia.

Kufuatia mabadiliko hayo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel amefika wilayani Misungwi na kukutana na moja ya kikundi cha wanawake ambacho kimehamasisha wanachama wake 10 kujenga nyumba za bati.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel (wa tano kushoto waliokaa), na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha Witogwa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel (wa tano kushoto waliokaa), na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanaharakati wa kujitolea ngazi ya jamii wanaosaidia kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel (wa tatu kulia aliokaa), na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja wanakikundi cha Witogwa wanaohamasisha ujenzi wa nyumba za bati na kuachana na nyumba za nyasi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel (wa tano kushoto waliokaa), na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanaharakati wa kujitolea ngazi ya jamii.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel akizungumza baada ya kukagua baadhi ya nyumba zilizojengwa na wanawake wilayani Misungwi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda akieleza mkakati wa wilaya hiyo kuhakikisha wananchi wanajenga nyumba za bati na kuachana na nyumba za nyasi.
Wanahabari wakipata ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Witogwa, Leah Buzuka namna walivyofanikiwa kujengeana makazi bora.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza na wanahabari kuhusiana na mchango wa shirika hilo katika kuhamasisha wananchi kujenga makazi bora.
Baadhi ya viongozi na wakazi wa Misungwi.
Baadhi ya viongozi na wakazi wa Misungwi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.