LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jahazi la Yanga laanza kuzama

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Bao pekee la mshambuliaji kutoka Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 86 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya vigogo Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye mchezo uliopigwa Aprili 25, 2021 kuanzia majira ya saa mbili usiku katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo Azam FC imefikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 28 ikibaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Yanga SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.

Mabingwa watetezi Simba SC wanaendelea kutawala kileleni kwa pointi 58 ikiwa imecheza mechi 25.
Via Binzubeiry Blog

No comments:

Powered by Blogger.