LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Aweso aacha sekeseke Sengerema, Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Maji, Juma Aweso ameeleza kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji Sengerema-Nyampande-Busulwangiri na kuagiza viongozi waliokuwa wanasimamia mradi huo kukamatwa ili kueleza ni kwa nini umekamilika lakini hautoi maji.

Waliokamatwa kwenye ziara hiyo iliyofanyika Aprili 25, 2021 ni Kaimu Mkurugenzi wa MWAUWASA Leonard Msenyele, Meneja RUWASA Mkoa Mkoa Mwanza Immaculata Raphael, Meneja RUWASA Wilaya Sengerema Kacian Wittike, Meneja Miradi MWAUWAS Godadi Mgwatu, Meneja SEUWASA Robert Lupoja pamoja na Mhandisi Mshauri.
Pia Waziri Aweso alivunja Bodi ya Mamlaka ya Maji Sengerema (SEUWASA).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Maji Juma Aweso (kulia) akiwasili wilayani Sengerema kwa ajili ya ukaguzi wa mradi wa maji. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya Sengerema Emmanuel Kipole (katikati).
Waziri wa Maji Juma Aweso akikagua tanki la kusambaza maji Sengerema-Nyampande-Busulwangiri.
Baadhi ya viongozi wa mamlaka za maji wakiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa kwa amri ya Waziri wa Maji Juma Aweso.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.