LIVE STREAM ADS

Header Ads

Msanii MMZY kutikisa na EP yake ya ASCENT

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ni nyota anaekuja kwa kasi ghini ya lebo ya Kerae Records, Akachukwu Emmanuel Uche maarufu kwa jina la Mmzy.

Anakuja vizuri kupitia muziki aina ya Afrobeat akiwakilisha nchini Naijeria. Licha ya msanii huyu kuwa na ubora katika uandishi wake, sauti yake ni moja ya kitu kinachomtofautisha na wasanii wengine ambao wamewahi kutokea katika muziki huko nchini Naijeria.

Mmzy ameachia rasmi Ep yake ya kwanza iliyopewa jina la "Ascent" yenye nyimbo nane huku ikiwa na kolabo mbili akiwa ameshirikiana na msanii wa muziki Teni pamoja na Teri.

Ascent Ep imetayarishwa na watayarishaji watano ambao ni Masterkraft, Echo The Guru, Cranker Mallo, Blaise Beats, Ozedikuz na nyimbo zote kukamilishwa na mtayarishaji Mix Monster.

Nyimbo zote zimeandikwa na msanii Mmzy isipokuwa aliyoshirikiana aa Teni na Terri bila kusahau wimbo namba 3, 4, 5 na 8.
Dominate ni moja ya wimbo wake unaofanya vizuri kwa sasa ukiwa unapatikana pia ndani ya Ep yake hiyo iliyopewa jina la Ascent.

Unaweza kuwa wa kwanza kusikiliza kazi zote kutoka kwenye EP kupitia vyanzo mablimbali ikiwemo Apple music, BoomPlay, Spotify, Audiomack na Youtube.

Vilevile kwa taarifa zaidi kuhusu Mmzy unaweza kumfuata kupitia ukurasa wake wa Instagram @therealmmzy

No comments:

Powered by Blogger.