LIVE STREAM ADS

Header Ads

Simba SC, timu bora Afrika kwa sasa, AS Vita wakubali yaishe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Timu ya soka Simba SC kutoka Tanzania imefuzu hatua ya Robo Fainali kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuitungua AS Vita Club kutoka Congo kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es salaam, Aprili 03, 2021.

Mchezo wa kwanza Simba SC iliitungua AS Vita ugenini bao 1-0, mchezo wa pili nyumba ikaitungua Al Ahly 1-0, mchezo wa tatu ugenini ikatoka 0-0 na El Merreikh, mchezo wa nne ikaitungua El Merreikh 3-1 kwa Mkapa na mchezo wa tano imeitungua AS Vita 4-1 kwa Mkapa.

Simba imefikisha jumla ya pointi 13 katika kundi A ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani wake kwenye kundi hilo huku ikiwa imesalia na mchezo mmoja wa ugenini dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Kwa mafanikio hayo wachambuzi wa soka wanaiweka Simba SC kwenye nafasi ya Klabu tano Bora barani Afrika kwa sasa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.