El Merreikh (Sudan) 0 - 0 Simba SC (Tanzania). Simba wana Bahati yao
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Timu ya soka ya Simba SC kutoka Tanzania imeendelea kujikita kileleni kwenye kundi A katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kutoka sare tasa na El Merreikh ya Sudan kwenye mchezo wao wa tatu.
Simba SC sasa imefikisha alama saba ikifuatiwa na AS Vita ya Congo yenye alama nne na wingi wa magoli ya kufunga, Al Ahly ya Misri yenye alama nne pia na El Merreikh ikiburuza mkia na alama moja kufuatia sare hiyo.
Mchezo wa kwanza Simba SC iliitungua AS Vita ugenini bao moja kwa mtungi, mchezo wa pili nyumba ikaitungua Al Ahly bao moja sufuri na mchezo wa tatu ugenini imetoka sare ya bila kufungana ugenini na El Merreikh, mchezo ambao Simba ilikuwa na bahati kubwa baada ya kukoswa koswa mara kadhaa na kuamua kubadili mbinu kwa kujilinda zaidi kuliko kushambulia.
SOMA>>> Habari zaidi kuhusu Simba
No comments: