LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa imeungana na wadau mbalimbali kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani 2021 ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 08 kwa lengo la kutambua mchango wa wanawake katika kuchochea shughuli za maendeleo katika jamii.

Hafla hiyo iliyowashirikisha pia baadhi ya wanawake ambao ni wateja wa CRDB imefanyika katika tawi la benki hiyo lililopo Rock City Mall jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya Nyamagana, mwanamama Dkt. Philis Nyimbi.

Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta amesema benki hiyo inathamini mchango wa wanawake na hivyo kuhakikisha inatoa huduma mbalimbali ikiwemo akaunti ya Malikia kwa lengo la kuunga mkono jitihada za wanawake katika kufikia malengo yao.

Naye Meneja wa CRDB tawi la Rock City Mall, Jesca Kikoito amesema maadhimisho hayo yanawakumbusha wanawake kutimiza wajibu wao huku wakipambana kwa ujasiri na kuonyesha uwezo walionao ili jamii itambue umuhimu wao katika kufikia usawa wa kijinsia wa asilimia 50 kwa 50.

Kwa upande wake mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi amesema ni jukumu la wanawake kupambana, kujitathmini na kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo bila kujali changamoto wanazokumbana nazo na kusonga mbele zaidi kimaendeleo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis Nyimbi (wa tatu kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wanawake mbalimbali jijini Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB Rock City Mall.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi (wa pili kushoto), Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta (kushoto), Meneja Biashara wa CRDB Kanda ya Ziwa Japhary Hassanary (wa pili kulia) na Meneja wa CRDB tawi la Rock City Mall Jesca Kikoito wakikata keki kama ishara ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2021.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta (kushoto) akimlisha keki mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi akimlisha keki Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Lusingi Sitta.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (kushoto) akimlisha keki Meneja wa CRDB tawi la Rock City Mall, Jesca Kikoito (kulia).
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (kulia) akimlisha keki Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly (kushoto).
Tazama picha mbalimbali mgeni rasmi na viongozi wa CRDB wakiwalisha keki wanawake/ wateja wa CRDB jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Meneja wa CRDB tawi la Rock City Mall, Jesca Kikoito (kushoto) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (kulia).
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.