Chama aandika historia nyingine “Simba vs AS Vita”
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
BMGHabari
Timu ya soka
ya Simba (Tanzania) imetinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya klabu
bingwa barani Afrika, baada ya kuitungua timu ya AS Vita (Congo) kwenye mchezo
uliopigwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, leo Machi 16, 2019 kuanzia
majira ya saa moja jioni.
Timu ya AS
Vita ilianza kupata goli la kwanza kupitia kwa Kazadi Kazengu dakika ya 13 ya
kipindi cha kwanza na baadaye Simba ikasawazisha kupitia kwa Mohammed Hussein dakika
ya 36.
Ule usemi wa
“kila mtu ashinde kwao” ulitimia dakika ya 90 baada ya Simba kupata goli la
ushindi kupitia kwa kwa Clatous Chama na hivyo kupelea vilio na majonzi kwa AS
Vita huku Chama akiweka historia nyingine kwa kuivusha Simba kama alivyofanya
katika hatua ya makundi alipofunga goli la ushindi dhidi ya Nkana kwenye uwanja
wa Taifa na kuiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-1.
Baada ya
ushindi wa leo, Simba wamefikisha pointi tisa kwenye kundi D wakitanguliwa na
Al Ahly wenye alama 10 baada ya ushindi wao dhidi ya JS Saoura goli 3-0 hii
leo. Nafasi ya tatu katika kundi hilo inashikwa na JS Soura wenye alama nane na
nafasi ya nne wakiwa ni AS Vita wenye alama saba.
No comments: