LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yatambua juhudi za shirika la TNDB kwenye utunzaji vyanzo vya Mto Nile

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Serikali ya Tanzania imesema inatambua kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Tanzania Nile Basin Discourse kwenye kutunza vyanzo vya mto Nile.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Bwana Salumu Kali kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya Bonde la mto Nile yaliyofanyika Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza Tanzania.

Kali alisema kuwa, Shirika la TNBD limekuwa likifanya kazi nzuri kwenye suala nzima la uhifadhi wa vyanzo vya mto Nile ukiwemo mto Simiyu, shughuli hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kwenye utunzaji wa mazingira.

Pia aliitaja jamii inayoishi pembezoni mwa mto Simiyu kuchukua hatua kwenye kulinda mto huo kwani bila kufanya hivyo watakuwa wanahatarisha uhai wa mto huo.

Donald Kasongi Mwenyekiti wa TNBD alisema maadhimisho hayo yamebebwa kauli mbiu ya tafakuri kwenye uwekezaji wa bonde la mto Nile, hivyo ni vyema jamii, serikali na wadau mbalimbali tukaungana kwenye kulinda vyanzo vya mto Nile.

Maadhimisho hayo yalifanyika April 20 mwaka huu katika Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza na kuhudhuriwa na zadi ya washiriki thelathini.
Na Martin Nyoni, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.