LIVE STREAM ADS

Header Ads

TBS yatoa mafunzo kwa wasindikaji mchele Bukombe, Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wa wilaya ya Bukombe yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba ameeleza kufurahishwa na mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.

Mhe. Nkumba ametoa pongezi hizo Jumatano Aprili 28,2021 wakati akifungua mafunzo hayo yaliyokutanisha wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele takribani 100 wa wilaya ya Bukombe.

Amesema mafunzo hayo ni njia muafaka ya kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,kilimo,biashara na maeneo mengine.

Ameongeza pia Mafunzo haya ni uthibitisho wa azma ya Serikali kupitia taasisi zake katika kufanikisha malengo ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo amewataka wadau wa mchele kutumia fursa ya mafunzo hayo kuongeza utaalamu katika uzalishaji na kuweza kuthibitisha ubora wa bidhaa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga amesema wadau wa mchele wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuzalisha bidhaa zilizokidhi viwango vya ubora na usalama.

Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala amesema TBS inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio ili kuleta ushindani na kukuza uchumi wa nchi.

Mafunzo hayo yameandaliwa na TBS na yamefanyika katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na yataendelea kwenye wilaya ya Katoro mkoani Geita na kumalizika katika wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza leo Aprili 28, 2021 wakati akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wa wilaya ya Bukombe yaliyotolewa na TBS kwa ajili kutoa elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na TBS kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akiishukuru na kuipongeza TBS kuendesha mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Kulia ni Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala akielezea lengo la TBS kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ambapo amesema ni kuhakikisha kuwa wanapata elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Joseph Ismail Mwaipaja akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.

No comments:

Powered by Blogger.