LIVE STREAM ADS

Header Ads

Milango yafunguliwa kwa washiriki "Lake Victoria Marathon" Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wanariadha nchini wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio za 'Lake Victoria Marathon' zinazotarajiwa kufanyika Juni 20, 2021 jijini Mwanza, zikilenga pia kuhamasisha utunzaji wa mazingira ya ziwa Victoria pamoja na utalii katika visiwa vilivyo katika ziwa hilo.

Baraka Nyororo ambaye ni mmoja wa waandaaji wa mbio za 'Lake Victoria Marathon' alitoa hamasa hiyo Mei 29, 2021 wakati wa uzinduzi wa mbio hizo ulioambatana na zoezi la kufanya usafi katika fukwe za ziwa Victoria ikiwemo 'Rock Beach' pamoja na kutembelea visiwa mbalimbali kama vile Saanane.

Naye Mratibu wa mbio hizo, Halima Chake alisema zoezi la wanadhiadha kujisajili linafanyika katika eneo la Rock City Mall ambapo washiriki wa kilomita 21 watachangia shilingi elfu 30 huku kilomita 10 na kilomita tano wakichangia shilingi elfu 20.

Aidha Chake alisema zawadi kwa washindi wa kwanza kilomita 21 wanaume na wanawake ni shilingi laki saba, wa pili shilingi laki tano, wa tatu shilingi laki tatu, wa nne na watano shilingi laki moja huku kilomita 10 mshindi wa kwanza akipata laki tano na wa pili shilingi laki tatu ambapo kilomita tano ni 'fun run' kwa ajili ya watoto.

"Sisi mbio hii tumeipokea kwa mikono miwili na kwa shangwe kubwa maana ni ya kwetu wana Mwanza, imekuja kuongeza fursa za uchumi kwetu wanariadha hivyo tujitokeze kwa wingi kujishiriki" alisisitiza Juma Maziku wakati akizungumza kwa niaba ya wanariadha kuhusiana na mbio za "Lake Victoria Marathon 2021".
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baadhi ya washiriki wa mbio za 'Lake Victoria Marathon' wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya usafi katika fukwe za ziwa Victoria jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa 'Lake Victoria Marathon' wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya usafi katika fukwe za ziwa Victoria.
Baadhi ya washiriki wa mbio za 'Lake Victoria Marathon' wakifanya usafi wa kuondoa taka za plastiki katika fukwe za ziwa Victoria.
Baadhi ya washiriki wa mbio za 'Lake Victoria Marathon' wakifurahia utalii ndani ya ziwa Victoria.
Washiriki wa mbio za 'Lake Victoria Marathon' wakiingia kwenye meli ya MV. Rafiki kuelekea kwenye hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Saanane.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.