LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jengo la abiria uwanja wa ndege wa Mwanza mbioni kukamilika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauro ya Jiji la Mwanza imetembelea ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kuelezwa kuwa mradi huo uko mbioni kukamilika.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Msimamizi wa mradi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Mhandisi Tunaye Mahenge (kulia) akitoa taarifa kwa Kamati ya Fedha na Uongozi kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilipotembelea mradi huo. Halmashauri hiyo pamoja na Manispaa ya Ilemela zimechangia gharama za ujenzi wa jengo hilo.
Msimamizi wa mradi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Mhandisi Tunaye Mahenge (kushoto) akifafanua jambo kuhusiana na ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi akiwemo Mtahiki Meya wa Jiji la Mwanza Costantine Sima (wa tatu kushoto), Naibu Meya Jiji la Mwanza Rodrick Ngoye (wa pili kushoto) wakimsikiliza msimamizi wa ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
Msimamizi wa mradi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza, Mhandisi Tunaye Mahenge (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya kutembelea mradi huo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.