LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya Equity yaja na mabadiliko makubwa kwa wateja wake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya kimataifa ya Equity imefanya mabadiliko ya nembo yake ili kuendana na huduma mbalimbali inazozitoa ikiwemo bima na mikopo yenye riba nafuu kwa wateja wake kuanzia wadogo, wa kati na wakubwa.

Akizungumza kwenye kongamano lililowakutanisha wateja wa benki hiyo jijini Mwanza, Mkurugenzi Mwendeshaji Benki ya Equity, Esther Kiteko alisema mabadiliko hayo yamekuja ili kuendana na maboresho ya huduma yaliyofanyika.

Kiteko alisema benki hiyo imepanua wigo zaidi wa kuwafikia wateja wake katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi na biashara ili kuwasaidia kutimiza malengo yao tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati inaanzishwa.

Naye mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi aliipongeza beki ya Equity kwa mabadiliko makubwa iliyoyafanya na kuhimiza uongozi wa benki hiyo kufanya kila jitihada ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Benki ya Equity Ilianzia nchini Kenya mwaka 1984 kama kikundi cha kusaidiana mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na baadae kutanuka katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati ambapo nchini Tanzania ilianza kutoa huduma za kifedha mwaka 2012.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi akifungua kongamano la benki ya Equity na wateja wake kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella. Dkt. Nyimbi aliipongeza benki ya Equity kwa juhudi zake za kufikisha huduma kwa wateja wapatao elfu 57,600 kupitia matawi, mawakala na mashine za kutolea fedha (ATM).
Meneja Benki ya Equity Tawi la Mwanza, Bahati Dollo alisema benki hiyo imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kuwawezesha wateja wake kupanua shughuli zao.
Meneja Benki ya Equity Tawi la Mwanza, Bahati Dollo akizungumza kwenye kongamano hilo lililofanyika Goldcrest Hotel jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mwendeshaji Benki ya Equity, Esther Kiteko alisema benki hiyo imeboresha pia imeboresha mwonekano/ nembo yake ili kuendana na mabadiliko makubwa ya huduma za kifedha iliyoyafanya kwa wateja wake.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.