LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uhaba wa samaki Ziwa Victoria waathiri viwanda Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Changamoto ya upatikanaji wa samaki katika Ziwa Victoria imeelezwa kusababisha uzalishaji wa viwanda vya kusindika minofu ya samaki jijini Mwanza, kushuka hadi kufikia tani 20 kwa siku kutoka tani 120 za hapo awali.

Hayo yamebainika Mei 23, 2021 wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kwenye viwanda vya Tanzania Fish Processors (TFP) pamoja na Victoria Perch vyote vyote vya jijini Mwanza.

Meneja Rasilimali Watu kiwanda cha TFP, Godfrey Samwel amesema hatua ya ukosefu wa malighafi kiwandani hapo imezorotesha usindikaji wa minofu ya samaki ikiwemo sangara ambao wana soko kubwa nje ya nchi na hivyo kulikosesha taifa mapato.

Amesema uhaba huo umesababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo wavuvi kutopeleka samaki viwandani baada ya kuibuka masoko ya ndani ya wanunuzi wa mabondo ya samaki katika maeneo ya visiwani na hivyo kuomba Serikali kuliwekea utaratibu mzuri suala hilo.

Naye Meneja Ubora kiwanda cha Victoria Perch, Edwin Okong’o amesema upungufu wa upatikanaji wa samaki katika Ziwa Victoria pia umesababisha na suala la uvuvi haramu na hivyo kuomba Serikali kuongeza mbinu za kudhibiti hali hiyo.

Kwa upande wake Afisa Uvuvi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kenedy Kitinusa amesema sababu nyingine iliyosababisha samaki kuadimika katika Ziwa Victoria ni mabadiliko ya hali ya hewa ambayo hutokea kila mweziFebruari na kusababisha vifo kwa samaki ambapo kwa mwaka huu hali ya vifo ilikuwa mbaya zaidi katika nchi zote, Tanzania, Kenya na Uganda.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri Ulega amesema Serikali inaandaa mfumo utakaodhibiti uvuvi haramu kuanzia kwa wazalishaji wa nyavu hadi kwa wavuvi huku pia akiwataka wamiliki wa viwanda kuchukua hatua zitakazowavutia wavuvi kutouza samaki kwa wanunuzi wa mabondo na badala yake kupeleka viwandani.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na uongozi wa kiwanda cha TFP jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Watendaji mbalimbali wa Wizara hiyo, akizungumza na uongozi wa kiwanda cha TFP.
Katibu Tawala Wilaya Nyamagana, Alfredy Yonas (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (hayuko pichani) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Philis Nyimbi. Kulia ni Meneja Biashara kiwanda cha TFP, Satendra Tiwari.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto) akimsikiliza Meneja Biashara kiwanda cha TFP, Satendra Tiwari (kulia).
Meneja Rasilimali Watu kiwanda cha TFP, Godfrey Samwel akiwasilisha taarifa ya uzalishaji wa kiwanda hicho.
Meneja Rasilimali Watu kiwanda cha TFP, Godfrey Samwel akiwasilisha taarifa ya uzalishaji wa kiwanda hicho.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kulia) akikagua minofu ya samaki iliyosindikwa katika kiwanda cha TFP kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto) akiwasili katika kiwanda cha TFP.
Viongozi wa kiwanda cha TFP (kulia) wakisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  alipowasili kiwandani hapo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto) akisamiliana na viongozi wa kiwanda cha TFP (kulia).
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (katikati) akiteta jambo na Meneja Rasilimali Watu Kiwanda cha TFP, Godfrey Samwel (kushoto). Kulia ni Katibu Tawala Wilaya Nyamagana, Alfredy Yonas.
Katibu Tawala Wilaya Ilemela, Said Kitinga (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Severine Lalika (hayuko pichani).
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kulia) akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Victoria Perch.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.