LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maendeleo ya Ujenzi wa Stendi ya Nyegezi Mwanza “kuna changamoto ilitokea”

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Imeelezwa kuwa ujenzi wa stendi ya kisasa ya Nyegezi iliyopo jijini Mwanza unaendelea vyema licha ya changamoto ya uhaba wa vifaa uliojitokeza hapo awali ambapo tayari umefikia asilimia 35 huku matarajio yakiwa ni kukamilika kwa wakati kulingana na muda wa mkataba.

Mradi huo wa kimkakati unatekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa shilingi bilioni 15.8 kutoka Serikali Kuu kupitia kampuni ya Mohammed Bulders ambapo ulianza Septemba 2020 ukitarajiwa kukamilika Aprili 2022 ikiwa na uwezo wa kubeba mabasi 120 kwa wakati mmoja, maduka 85, kumbi za burudani na maeneo matatu ya abiria kukaa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
  
Mwonekano wa stendi ya Nyegezi itakapokamilika.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.