LIVE STREAM ADS

Header Ads

Halmashauri mkoani Mwanza zanyoshewa kidole

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Halmashauri mkoani Mwanza zimetakiwa kutenga bajeti kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa shughuli za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo kutokomeza mimba kwa wanafunzi wa kike.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emil Kasagala wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi na salama wa Wanawake na Watoto mkoani Mwanza na kuongeza kuwa ukosefu wa bajeti inayopaswa kutengwa na halmashauri kimekuwa kikwazo kikubwa kwa kamati hiyo kutekeleza vyema majukumu yake.

Kasagala alisema kuna Halmashauri mkoani Mwanza hazitekelezi mikakati ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ikiwemo MTAKUWWA kwa kisingizio cha ukosefu wa bajeti na hivyo kukwamisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukati wa kijinsia.

"Niziagize Halmashauri za Mkoa Mwanza kutenga bajeti hata kwa kutumia mapato ya ndani ili kuwezesha shughuli za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika ngazi zote hadi vijijini" alisisitiza Kasagala.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isaac k Ndasa alitoa rai kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto mkoani humo kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoripotiwa katika jamii na hivyo kuokoa gharama nyingi zinazotumika kwenye mapambano hayo na kuzihamishia kwenye miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawakena watoto (KIVULINI), Yassin Ally alisema jitihada za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji bado zinakwamishwa na baadhi ya vyombo vya maamuzi ikiwemo mahakama kwa kufuta mashauri mengi kwa kigezo cha kukosa ushahidi wa kutosha na hivyo kuomba eneo hilo kufanyiwa kazi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Emil Kasagala (aliyesimama) akifungua kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto mkoani Mwanza.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isaac k Ndasa (aliyesimama) akieleza jitihada mbalimbali zinazofanywa kutokomeza ukatili wakijinsia mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akieleza mchango wa shirika hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsia mkoani Mwanza.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto na Wanawake Mkoa Mwanza pamoja na wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho.
Wadau mbalimbali wakiwemo wa mahakama wakifuatilia kikao hicho.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto mkoani Mwanza.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Mwanza wakifuatilia kikao hicho.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.