LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyimbi atatua mgogoro uliotishia usalama Nyamagana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Kamati Maalumu iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya Nyamagana mkoani Mwanza, Dkt. Philis Nyimbi ili kuchunguza mgogoro wa umiliki wa ardhi katika Mtaa wa Sweya Kata ya Luchelele wilayani humo imekamilisha jukumu lake.

Mgogoro huo uliodumu tangu mwaka 2019 ulihusisha Serikali ya Mtaa wa Sweya na mkazi wa mtaa huo ambapo pande zote mbili zilikuwa zikidai kumiliki eneo hilo hatua iliyomlazimu DC Nyimbi Disemba 08, 2020 kuunda Kamati ili kuchunguza mmiliki halali.

Baada ya Kamati hiyo kumaliza jukumu lake iliwasilisha ripoti kwa DC Nyimbi ambaye Mei 07, 2021 alifika katika Mtaa huo na kueleza bayana mmiliki halali wa eneo hilo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.