LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Biteko aweka jiwe la msingi kwenye Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Geita

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kisasa cha kusafisha dhahabu mkoani Geita (Geita Gold Refinery- GGR) ambacho ujenzi na usimikaji mitambo umekamilika kwa asilimia 99.

Biteko ameweka jiwe hilo Mei 08, 2021 na kumpongeza mwekezaji mzawa wa kiwanda hicho kwa uwekezaji alioufanya kwani utafungua fursa zaidi katika soko la madini hususani kwa wachimbaji wadogo.

Alisema ujenzi wa kiwanda hicho ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya madini iliyotaka madini yote kuongezewa thamani hapa nchini na si kusafirishwa kwenda nje ya nchi kama madini ghafi na hivyo kwenda kunufaisha viwanda vya mataifa mengine.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya kiwanda cha GGR, Athuman Mfutakamba alisema ujenzi wa kiwanda hicho umegharimu dola  milioni nane na kwamba kitakuwa na uwezo wa kusafisha dhahabu hadi kufikia Kg 440 kwa siku kwa kiwango cha asilimia 99.99 na hivyo kutenganisha madini mengine kama shaba yanayokuwa kwenye dhahabu.

Kiwanda cha kusafisha dhahabu Geita ni miongoni mwa viwanda vitatu vilivyojengwa nchini kikiwemo cha Mwanza na Dodoma ambapo kwa pamoja vitapanua wigo wa soko la madini, kuongeza mapato ya Serikali, wachimbaji na wafanyabiashara wa madini na hata kudhibiti utoroshaji madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akimpongeza Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi obert Gabriel (kushoto) kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu mkoani humo.
Mkurugenzi wa Bodi ya kiwanda cha GGR Athuman Mfutakamba (kushoto) akitoa ufafanuzi wa Waziri wa Madini (Doto Biteko (katikati) kuhusiana na ujenzi wa kiwanda hicho. Kulia ni Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu kulia) na viongozi mbalimbali wakipata ufafanuzi kuhusiana na ujenzi wa kiwanda cha kusaisha dhahabu mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akis
Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Madini, Doto Biteko wakisikiliza ufafanuzi kuhusiana na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa sita kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Mwonekano wa kiwanda cha kusafisha dhahabu mkoani Geita (GGR). Kiwanda hicho kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.