LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanaume wasidhani hatutaki wawe viongozi- TAMWA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimetoa rai kwa wanajamii kubadilika na kukubali ushiriki wa wanawake katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo nafasi za kisiasa.

Rai hiyo imetolewa jijini Mwanza Mei 20, 2021 na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Rose Reuben wakati akifungua warsha ya waandishi wa habari kutoka redio za kijamii Kanda ya Ziwa iliyolenga kutoa mrejesho kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa "Wanawake Wanaweza, Wape Nafasi" unaotekelezwa na TAMWA kwa ufadhili wa shirika la UN Women.

Amesema jamii inapaswa pia kuwashirikisha wanawake katika maamuzi mbalimbali ikiwemo ya kisiasa hatua itakayosaidia maamuzi yanayotolewa kuwa na usawa huku akiongeza jamii hususani wanaume wasithani TAMWA na mashirika mengine yanayosisitiza uwepo wa wanawake katika uongozi haitaki wanaume kuwa katika uongozi bali inatamani kuona usawa katika kila nyanja kama ilivyo kwa Rais wa Tanzania (mwanamke) na Makamu wa Rais (mwanaume).
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben akizungumza kwenye 
Washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Rose Reuben wakati akifungua warsha hiyo.
Mwanahistoria wa Mambo ya Kale, Ibengwe Shileki akieleza namna alivyoshiriki kwenye utekelezaji wa mradi wa Wanawake Wanaweza, Wape Nafasi katika kuelimisha jamii kuwaunga mkono wanawake katika kuwania nafasi za uongozi katika jamii.
Katika hafla hiyo, waandishi wa habari kutoka redio za kijamii wamehimizwa kuendelea kuandaa vipindi vinavyowawezesha wanawake kushiriki katika shughuli za uongozi na maamuzi ili kufikia usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Rose Reuben (kushoto) akiteta jambo na Mwanahistoria wa Mambo ya Kale, Ibengwe Shileki (kulia) ambaye pia alishiriki utekelezaji wa mradi wa Wanawake Wanaweza.
Mwakilishi kutoka redio Kahama FM, Christina Christian (kushoto) akieleza namna vipindi vilivyoandaliwa na redio za kijamii vilichochea wanawake kuthubutu na kuwania nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, mwaka jana 2020.
Meneja Mipango TAMWA, Sylivia Daulinge akiongoza majadiliano kwenye warsha hiyo ambapo alisisitiza wanahabari kutoka redio za kijamii kuwashirikisha wanawake kwenye habari, makala na vipindi mbalimbali vyenye kuchochea hamasa ya wao kuwania nafasi za uongozi.
Washiriki wa warsha hiyo (kushoto) wakifurahia wasilisho kutoka kwa Meneja Mipango TAMWA, Sylivia Daulinge (kulia).
Washra hiyo imewajumuisha washiriki kutoka mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga.
Washiriki wa warsha hiyo wakichangia mada...
Picha ya pamoja
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.