LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA wamaliza kazi, wapanga safu mpya BAWACHA

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Baada ya kumwondoa Halima Mdee na wezake 18, Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) limemchagua Catherine Ruge kuwa Katibu Mkuu kwa ushindi wa kura 34 dhidi kura 23 alizopata mshindani wake wa karibu, Ester Daffi.

Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Asia Msangi amepata kura nane ambazo hazikutosha kumpa uongozi alioumba kwa makada wenzake.

Wakati Catherine akiibuka mshindi wa nafasi hiyo ya juu, Bahati Chumu Haji amechaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ambaye alikuwa mgombea pekee kwa kupata kura 60 za ndiyo na tano za hapana.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jijini Mwanza Mei 18, 2021, Ruth Mollel aliyekuwa msimamizi amemtaja Nuru Ndossi kuwa mshindi wa nafasi ya unaibu Katibu Mkuu Bara kwa kupata kura 33.

Nuru alichuana na Brenda Rupia aliyeondoka na kura 17 na Emma Bhoki aliyepata kura 15. Nafasi nyingine iliyopata kiongozi ni Matibu Uenezi wa Bawacha Taifa ambapo amechaguliwa Aisha Machano Amme aliyepata kura 36 hivyo kumshinda Husna Said aliyepata kura 23.

Uchaguzi huo wa BAWACHA umefanyika ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi baada ya baadhi wa waliokuwa viongozi kuvuliwa uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama.

Licha ya msimamo huo wa chama, Spika wa Bunge, Job Ndugai ameendelea kuwatambua akisema hakuna utaratibu uliokiukwa ndani ya chama hichio kilichokuwa kinaongoza kwa idadi kubwa ya wabunge wa upinzani kwenye Bunge la 11.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.