LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wachimbaji Madini watakiwa kutumia mafunzo yanayotolewa na GST

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wa madini nchini kuyatumia vyema mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuboresha shughuli zao na kuzalisha kwa tija.

Biteko alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita na kuongeza kuwa ni vyema wakazingatia pia sheria na kanuni za usalama mahali pa kazi ili sekta ya madini iwe na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Aidha aliwasihi wachimbaji wadogo wa madini kuyatumia masoko ya madini yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali nchini kuuza madini yao huku wakiacha utoroshaji madini, kutoa taarifa na kukemeana wenyewe wanapoona mwenzao anajihusisha na vitendo vya utoroshaji madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akisikiliza jambo wakati wa mafunzo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachimaji Madini Mkoa Geita.
Kaimu Mtendaji Mkuu GST Yokbeth Muyumbilwa (katikati), Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kulia) na Mratibu wa Mafunzo kutoka GST Dominic Kalimenze (kushoto) wakifuatilia wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.