LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Magu kupambana na tatizo la mimba kwa wanafunzi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Magu mkoani Mwanza, Salum Kalii ameahidi kulivalia njuga suala la kuwapima ujauzito wanafunzi katika shule mbalimbali wilayani humo na kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote hatua itakayosaidia kupambana na changamoto hiyo.

Kali alitoa kauli hiyo Mei 11, 2021 kwenye kongamano la kutafuta mbinu za kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Magu lililowashirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali za Vijiji, Kata, Halmashauri na dawati la jinsia la polisi.

Alisema wanafunzi watakaobainika kuwa na ujauzito pamoja na wazazi wao atahakikisha anawahifadhi mahali ambapo hawataharibu ushahidi kama ambavyo imekuwa ikijitokeza kwa baadhi ya wazazi na wanafunzi wenye ujauzi kurubuniwa na kuharibu ushahidi wa kuwatia hatiani wenye tabia ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

Aidha Kalii aliwataka wenyeviti wa Vitongoji na Kijiji kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kwa wanaowarubuni wanafunzi wa kike kimapenzi na kuonya kuwa atawachukulia hatua watakaoshindwa kuwajibika.

Naye Afisa Mtendaji Mamlaka ya Mji Mdogo wa Magu, Fundikira Said alisema ili kupambana na changamoto ya mimba kwa wanafunzi wa kike, ni vyema wazazi wakashiriki ipasavyo katika kuchangia gharama za chakula mashuleni hatua itakayosaidia kuwanusuru na vishawishi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wananwake na watoto (KIVULINI), Yassin Ally alisema matukio ya wanafunzi kupata ujauzito wilayani Magu yanashtua na mbaya zaidi baadhi ya waalimu wakituhumiwa kujihusisha kimapenzi na wanafunzi ambapo aliomba mamlaka husisha kuchunguza na kuchukua hatua.

Kwa mujibu wa dawati la jinsia la polisi wilayani Magu, wanafunzi wa kike 25 wamepata ujauzito hatua iliyowashtua viongozi na wadau mbalimbali na hivyo kukukata kuweka mikakati yakupambana na changamoto hiyo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalii akizungumza kwenye kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalii.
Afisa Mtendaji Mamlaka ya Mji Mdogo wa Magu, Fundikila Said akisisitiza wazazi kuwajibika ili kuwanusuru wanafunzi na vishawishi hususani kuchangia chakula mashuleni.
Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Magu, Simon Mpandalume akizungumza kwenye kikao hicho na kuwahimiza viongozi wa serikali za vitongoji na vijiji kuhamasisha wazazi kuchangia ujenzi wa shule za Sekondari ili kuwasaidia wanafunzi kutotembelea umbali mrefu kusaka elimu.
Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally akichangia hoja kwenye kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Kongamano hilo liliandaliwa na shirika la KIVULINI.
Viongozi mbalimbali wilayani Magu wakiwa kwenye kongamano la kujadili mbinu za kupambana na ukatili kwa wanawake na watoto.

No comments:

Powered by Blogger.