LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko atishia kuyafunga machimbo ya Nyakafuru Geita ‘acheni la manyani’

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Madini, Doto Biteko ametishia kuyafunga machimbo ya Nyakafuru Wilaya Mbogwe mkoani Geita ikiwa mgogoro wa umiliki wa mashamba hautafikia mwisho. Biteko amewaonya wanaodai umiliki wa mashamba kuacha kuwasumbua wachimbaji.

Aidha Waziri Biteko alisema Wizara yake haitatoa leseni katika machimbo hayo ambayo kwa sasa yanasimamiwa na kikundi cha wachimbaji wadogo Isanjabadugu hadi wananchi wanaodai kumiliki mashamba katika eneo hilo watakapomaliza mgogoro wao wa umiliki.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo ya Nyakafuru wilayani Mbogwe wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko.
Waziri wa Madini, Doto Biteko na viongozi mbalimbali akikagua baadhi ya maduara katika machimbo ya Nyakafuru Wilaya Mbogwe mkoani Geita.
Machimbo ya dhahabu ya wachimbaji wadogo Nyakafuru wilayani Mbogwe yanasimamiwa na kikundi cha Isanjabadugu ambapo wachimbaji hao wametakiwa kucha migogoro hatua itakayowawezesha kupatiwa leseni na Wizara ya Madini.
Baada ya umeme kufika katika machimbo ya Nyakafuru wilayani Mbogwe, baadhi ya maduara yanatumia nishati hiyo kwenye shughuli za ushimbaji ikiwemo kutolea mawe shimoni kwa kutumia mashine.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.