LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia azindua kiwanda cha dhahabu Mwanza, aagiza usimamizi thabiti

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Madini kupitia kwa Waziri wake Doto Biteko kuimarisha mfumo wa usimamizi wa madini nchini na kudhibiti utoroshaji ili kuhakikisha Taifa linanufaika.

Rais Samia ametoa agizo hilo Juni 13, 2021 wakati akizindua kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza kilichojengwa kwa ubia baina ya kampuni Rozella ya Dubai, PTE ya Singapore pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa gharama ya shilingi bilioni 12.2.

Aidha Rais Samia ameiagiza Wizara hiyo yenye dhamana ya madini kuanza mchakato wa kuboresha nembo (Rebrand) ya madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee ili kuyapa thamani yake.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.